Watoto waangukiwa na ukuta Katavi, mmoja afariki
12 April 2024, 8:55 pm
Nyumba ambayo ukuta wake umeanguka na kuwaangukia Watoto Wawili ambapo Mmoja kati yao amefariki .Picha na Deus Daud
“Baada ya Mvua Kunyesha na Maji kuwa mengi yamezunguka Nyumba na kusababisha kuanguka kwa Ukuta wa Nyumba hiyo“
Na Lilian Vicent -Katavi
Mtoto Mmoja Mwenye Umri wa Miaka Mitano amepoteza Maisha na Mwingine amepata Majeraha baada ya kuangukiwa na Ukuta wa Nyumba waliyokuwa wakiishi kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa.
Wakizungumza na Mpanda Redio Fm Mashuhuda Wa tukio hilo lililotokea Mtaa Kapalangao Kata ya Kazima Mkoani Katavi wamesema baada ya Mvua kunyesha na Maji kuwa Mengi yamezunguka Nyumba na kusababisha kuanguka kwa Ukuta wa Nyumba hiyo.
Sauti za Mashuhuda Wa tukio hilo lililotokea Mtaa Kapalangao Kata ya Kazima
Kwa upande wake Mama Mzazi wa Watoto hao Zainabu Hamimu ameeleza kuwa Watoto wake walikuwa wamelala wakati Mvua ikinyesha kabla ya tukio hilo kutokea .
Sauti ya Mama Mzazi wa Watoto Walioangukiwa na Ukuta akieleza Tukio lilivyokuwa
Nae Diwani wa kata ya Kazima Linus Evarist amesema alipokea Taarifa ya tukio hilo na baadae alifika eneo la tukio kwenda kushuhudia na ameongeza kuwa Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimechangia kwa kiasi kikubwa Ukuta wa Nyumba hiyo Kuanguka .
Sauti ya Diwani wa kata ya Kazima Linus Evarist akilielezea Tukio hilo
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Kaster Ngonyani ametoa wito kwa Wakazi wa Maeneo hayo kuchukua Tahadhari hususani katika kipindi hiki cha Mvua.
Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akithibitisha tukio hilo
Ikumbukwe kuwa Tukio hilo limetokea usiku wa April 8 Mwaka huu Mtaa wa Kapalangao kata ya Kazima mkoani Katavi kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa na kuleta athari katika baadhi ya Maeneo.Ili kuitazama Video ya taarifa hii bonyeza hapa