RC Katavi: Serikali inatambua umuhimu wa Vvongozi wa dini
12 April 2024, 8:21 pm
Picha na Mtandao
“Amewapongeza viongozi wa Baraza la BAKWATA kwa kuonyesha Ushirikiano katika juhudi zinazofanywa na Serikali na kuainisha kuwa Serikali inatambua Mchango wa Dini katika kufanya Shughuli za Maendeleo “
Na Samwel Mbugi-Katavi
Viongozi wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania ( BAKWATA) Mkoa wa Katavi wametoa Shukrani kwa Mkuu wa Mkoa na Viongozi Wote wa Wilaya kwa Ushirikiano Waliouonyesha katika kutekeleza Shughuli za imani katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akisoma Risala Wakati wa Baraza la Sikukuu ya Eid- Al- Fitr lililofanyika Ukumbi wa Manispaa iliyoandaliwa na Ofisi ya BAKWATA mkoani hapa Mbele ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko, Katibu Mkuu wa BAKWATA Mkoa wa Katavi Omary Muna ameshukuru kwa Ushirikiano wanaopatiwa na Serikali katika kutimiza Shughuli zao za Kiimani.
Sauti ya Katibu Mkuu wa BAKWATA Mkoa wa Katavi Omary Muna akizungumza
Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewapongeza Viongozi wa Baraza la BAKWATA kwa kuonyesha Ushirikiano katika Juhudi zinazofanya na Serikali na kuainisha kuwa Serikali inatambua Mchango wa Dini katika kufanya Shughuli za Maendeleo kwa jamii ikiwemo kujenga Shule na Vituo vya Afya
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akiwapongeza Viongozi wa BAKWATA
Katika hatua nyingine Mrindoko amewataka Wananchi kuchukua Tahadhari katika kipindi hiki cha Mvua zinazoendelea kunyesha hususani Wananchi wanaoishi sehemu za Mabondeni na kutoa pole kwa Wananchi waliopata Changamoto kufuatia Mvua zilizonyesha siku za hivi Karibuni.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizunguza na Wananchi kuhusu kuchukua Tahadhari ya Mvua zinazoendelea kunyesha
Hata hivyo ameziagiza Taasisi zote zinazohusika na Swala la Barabara kuchukua Tahadhari ya Uchunguzi wa Miundombinu ya Madaraja ndani ya Mkoa wa Katavi.