Bilioni 16 zatengwa ujenzi umeme gridi ya taifa Tabora-Katavi
10 April 2024, 11:24 pm
Picha na Mtandao
“Wakandarasi wanaohusika na ujenzi huo kutokana na kasi ya ujenzi na kuwataka kuuongeza ufanisi wa ujenzi ili kuweza kuukamilisha kwa wakati”
Na Betold Chove-Katavi
Kiasi cha Bilioni 16 zimetengwa na serikali kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa umeme wa Gridi ya Taifa kutoka mkoani Tabora hadi mkoani Katavi
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko alipotembelea na kujionea Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo wa Umeme.
Mrindoko Amewapongeza Shirika la Umeme Tanzania pamoja na Wakandarasi wanaohusika na Ujenzi huo kutokana na Spidi ya Ujenzi na kuwataka kuuongeza ufanisi wa Ujenzi ili kuweza kuukamilisha kwa wakati.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akielezea mradi huo
Katika hatua nyingine Mrindoko amewataka kuhakikisha mradi huo unakamilika kufikia tarehe 30 June Mwaka 2024 na hakutakuwa na muda wa ziada utakaotolewa baada ya Muda huo kupita
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza na kutoa maagizo kuharakisha Mradi huo ili ukamilike kwa wakati