Mkoa wa Katavi umepokea Fedha zaidi ya Trillion Moja kutoka kwa Serikali
8 April 2024, 3:07 pm
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko .Picha na Mtandao
“Mafanikio ya Mkoa wa Katavi kwa miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia“
Na Liliani Vicent -Katavi
Mkoa wa Katavi umepokea Fedha zaidi ya Tshs Trillion Moja kutoka kwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha huduma za Kijamii na kutatua Kero za Wananchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati wa Kongamano kuhusu Mafanikio ya mkoa wa Katavi kwa Miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza katika kungamano hilo
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesema kupitia Fedha zilizotolewa na Serikali Wananchi wameweza kupata Mradi wa Maji na kutatua Kero iliyokuwa imedumu kwa Muda Mrefu.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu
Nao Baadhi ya Wananchi walioudhuria kongamano hilo wamesema katika Miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya Sita wameona Mafanikio yaliyofanyika katika Sekta Mbalimbali .
Sauti za Wananchi waliohudhuria kongamano hilo wakitoa shukrani zao kwa mafaniko katika kipindi cha Miaka mitatu ya Uongozi wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia suluhu Hassain