Wananchi Mkoani Katavi Wasisitizwa Kupima Ugonjwa wa Kifua Kikuu
4 April 2024, 3:54 pm
Mratibu wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Bruno Cronely.picha na Samwel Mbugi
“Mtu yoyote mwenye ugonjwa unaoweza kupelekea upungufu wa kinga za mwili, ni rahisi kupata kifua kikuu”
Na Samwel Mbugi-Katavi
Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wametoa maoni mseto kuhusiana na ugonjwa wa kifua kikuu ambao umeonekana kuwa hatari katika jamii.
Hayo yamesema na baadhi ya wananchi ambao wamezungumza na Mpanda Redio Fm, kuwa Ugonjwa huo umekuwa na dalili tofauti, ambapo Miongoni ,Mwa dalili ni kukohoa mara kwa mara na kutokwa na jasho nyakati za Usiku.
Wameendelea kusema kuwa mamlaka husika zinatakiwa kutoa elimu ya mara kwa mara ili Wananchi wengi waweze kujua namna ya kujikinga na Ugonjwa huo .
Sauti za Wananchi wakieleza namna wanavyoufahamu ugonjwa wa kifua kikuu na jinsi ya kujikinga
Kwa upande wake Mratibu wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Bruno Cronely amesema kuwa mwaka 2023 waliweza kuibua Wagonjwa takribani 517 waliougua kifua kikuu.
Sauti ya Mratibu wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Bruno Cronely
Katika hatua nyingine amesema kuwa mtu yoyote mwenye Ugonjwa unaoweza kupelekea upungufu wa kinga za Mwili, ni rahisi kupata kifua kikuu.
Sauti ya Mratibu wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Bruno Cronely akieleza upungufu wa Kinga Mwilini unavyoweza kuleta uwezekano wa kupata kifua kikuu
Mratibu wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Bruno Cronely.picha na Samwel Mbugi
Hata hivyo Bruno amewataka wananchi wanaohisi kuwa na dalili za Ugonjwa huo kupima ili kuepusha Maambukizi Mapya katika jamii.