Zaidi ya Vitambulisho Elfu 64 vya NIDA Vyaletwa Mpanda
22 March 2024, 2:24 pm
“Wananchi amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kwani vimewaondoa hofu ya kukosa huduma muhimu ambazo zinaambatana na vitambulisho vya taifa kama vile kufungua akaunti za Benk“ Picha na Samweli Mbugi
Na Samweli Mbugi-katavi
Wananchi wa kata ya Mwamkulu Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamefurahishwa na uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya taifa [Nida] kwa awamu ya pili uliofanya katika kata hiyo.
Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wamesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia kwani vimewaondoa hofu ya kukosa huduma muhimu ambazo zinaambatana na vitambulisho vya taifa kama vile kufungua akaunti za Benk.
Sauti za wananchi wa kata ya Mwamkulu walipokuwa wakizungmza baada ya ujio wa vitambulisho hivyo.
Wananchi wa kata ya Mwamkulu waliohudhuria katika halfla ya kukabidhi vitambulissho hivyo. Picha na Samweli Mbugi
Aidha Afisa usajili wa vitambulisho vya taifa Wilaya ya Mpanda Mauna Karumbeta wakati akisoma taarifa ya vitambulisho hivyo amesema kuwa wamepokea jumla ya vitambulisho 64,596 ambavyo vitagawiwa kwa kila kata huku zoezi hilo la ugawaji litasimamiwa na watendaji wa kata husika.
Sauti ya Afisa usajili wa vitambulisho vya taifa Wilaya ya Mpanda Mauna Karumbeta.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Mpanda ambae pia ni mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya taifa Geofrey Mwashitete amesema kuwa kuna umuhimu kwa kila mwananchi apate kitambulisho cha taifa kwani kinafaida kwenye shughuli za kila siku.
Sauti ya katibu tawala wa wilaya ya Mpanda Geofrey Mwashitete
Mwashitete ameongezea kwa kuwaagiza watendaji wote ndani ya Wilaya ya Mpanda kwa kutoa wiki moja kila mwananchi apate kitambulishio hicho huku zoezi hilo liendelee kusimamiwa na madiwani wa kata husika.