Baraza la madiwani Tanganyika lapitisha mapendekezo ya bajeti bil. 33
16 February 2024, 11:58 pm
Picha na Festo Kinyogoto
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Hamad Mapengo amesema bajeti hiyo inakwenda kutatu changamoto mbalimbali huku nguvu kubwa ikiwa imeelekezwa katika sekata ya Elimu na Afya.
Na Leah Kamala-Katavi
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika limeridhia kupitisha bajeti Zaidi ya shilingi bilioni 33, kwaajili ya utekelezaji wa shughuli mablimbali za kimaendeleo Katika Wilaya hiyo kwa mwaka 2024-25.
Akitoa uthibitisho wa mapendekezo ya bajeti hiyo mbele ya baraza la Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Hamad Mapengo amesema bajeti hiyo inakwenda kutatua changamoto mbalimbali huku nguvu kubwa ikiwa imeelekezwa katika sekata ya Elimu na Afya.
Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Hamad Mapengo akitoa uthibitisho wa bajeti hiyo.
Awali akisoma bajeti hiyo Afisa Mipango wilaya ya Tanganyika Deus Ruziga amesema kiasi cha shilingi bilioni 9.5 ni mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi bilioni 18, 216 ni mapato kutoka serikalini na shilingi bilioni 5 ni ni fedha kutoka serikalini kwajili ya miradi ya maendeleo.
Sauti ya Afisa Mipango wilaya ya Tanganyika Deus Ruziga akisoma rasimu ya bajeti hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Dokta Alex Mrema amesema Watahakikisha watendaji wa sekta zote wanatimiza majukumu na ameshauri madiwani kupewa uelewa juu ya shughuli zote ambazo zinatekelezwa na wataalamu wa sekta mbalimbali.
Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Dokta Alex Mrema akichangia wakati wa baraza hilo la kupitia na kupitisha bajeti.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Dokta Alex Mrema alipokuwa akichangia hoja. Picha na Festo Kinyogoto
Baadhi ya watendaji wa sekta mbalimbali na wageni waalikwa waliohudhuria baraza hilo la kupitia na kupitisha rasimu ya bajeti wakisikiliza na kuchangia hoja.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka watendaji wa sekta zote kushirikiana na Madiwani katika kuendelea Kutatua changamoto huku akimuagiza meneja wa Ruwasa wilayani humo kuhamishia Ofisi zao kutoka mjini kwenda huko ili wakawahudumie Wananchi wa ufanisi.