Mpanda-Wananchi msitelekeze wagonjwa hospitali
9 February 2024, 3:08 pm
Baadhi ya wagonjwa wanaofikishwa katika hospital Hutelekezwa na ndugu zao na kuleta mzigo kwa serikali.Picha na Mtandao
Na Veronica Mabwile-Katavi.
Wito umetolewa kwa wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kuacha taabia ya kuwatelekeza wagonjwa wakati wakupatiwa huduma za matibabu ili kuipunguzia mzigo.
Wito huo umetolewa na Mganga mfawidhi hospital ya Manispaa ya mpanda DK PAUL LUGATA wakati akiongea na kituo hiki na kusema kuwa wapo baadhi ya wagonjwa wanaofikishwa katika hospital hiyo na kutelekezwa na ndugu zao na kuleta mzigo kwa serikali.
Sauti ya Mganga mfawidhi hospital ya Manispaa ya mpanda DK PAUL LUGATA.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa chanzo cha wagonjwa kutelekezwa wakati wa kupatiwa na matibabu inatokana na hali duni ya uchumi kumudu gharama za matibabu sambamba na kupungua kwa hali ya kujali kwa baadhi ya wanajamii.
Sauti ya wananchi wakieleza kuhusu sababu za kutelekeza wagonjwa hospitali
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii katika hospital hiyo ANIRUMI LONGO amesema kuwa niwajibu wa jamii kushirikiana na serikali ili kuwasaidia Wwagonjwa ambao wanapitia changamoto za kiuchumi wakati wa matibabu.
Sauti ya afisa ustawi wa jamii katika hospital hiyo ANIRUMI LONGO.
Kumekuwepo kwa changamoto ya baadhi wagonjwa kutelekezwa katika vituo vya afya na hospitali jambo ambalo limekuwa likiibua mkanganyiko kwa watoa huduma .