DC Mpanda: Waliofyekewa mahindi walipwe
5 February 2024, 4:14 pm
“Chama Cha Mapinduzi hakipo tayari kuona baadhi ya wananchi wakidhurumiwa haki zao.Picha na Deud Daud
Na Festo Kinyogoto
Mjumbe wa halamashauri kuu ya CCM taifa, katibu wa itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi PAUL MAKONDA Amemuagiza mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph Kuwalipa fidia wananchi waliofyekewa mahindi kata ya Mpanda hotel Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Ametoa maagizo hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kashaulili ambapo amesema Chama Cha Mapinduzi hakipo tayari kuona baadhi ya wananchi wakidhurumiwa haki zao.
Sauti ya Awali Mjumbe wa halamashauri kuu ya CCM taifa, katibu wa itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi PAUL MAKONDA
Wakitoa malalamiko mmoja wa Wananchi aliefyekewa Mahindi amesema wamefuatilia kwa muda mrefu kutaka kujua hatima ya kupata fidia kwani zoezi lilipositishwa mkuu wa wilaya aliahidi kutoa fidia ambayo wamezungushwa kwa muda mrefu.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Mpanda Joseph lwamba amesema alipokea malalamiko ya wananchi hao kufyekewa mahindi n alipojaribu kufuatilia zoezi hilo alibaini yapo Mahindi katika eneo la Manispaa ambayo hayajafyekwa na chama cha mapinduzi hakikuwa na taarifa juu ya zoezi hilo.
Sauti ya Mwenyekiti wa ccm Wilaya ya Mpanda.