ULEGA: TUMIENI MAFUNDISHO KULETA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA MAZIWA NCHINI
8 June 2022, 3:34 pm
Naibu waziri wa kilimo na uvuvi Abdala Ulega Amezitaka jamii mkoani Katavi kutumia mafundisho waliyoyapata katika maadhimisho ya wiki ya maziwa ili kuleta mabadiliko katika sekta ya maziwa nchini.
Akizungumza wakati wa kufunga wiki ya maziwa mkoani hapa Ulega amesema kuwa serikali imewekeza pesa kwa mwaka wa pesa 2022/2023 katika sekta ya maziwa ambapo million 120 zitatumika kuanzisha kituo cha ukusanyaji maziwa katika manispaa ya mpanda .
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua hoza mrindoko amewataka wananchi wa katavi kutumia fursa zilizojitokeza katika maadhimisho katika kukuza uchumi wa wafugaji pamoja na uchumi wa mkoa .
Maadhimisho ya 25 ya wiki ya ya Maziwa kitaifa yamefungwa june 1 mkoani hapa na naibu waziri wa kilimo na uvuvi abdala ulega huku yakiwa na kaulimbiu isemayo Kunywa Maziwa yaliyosindikwa Tanzania , lishe bora na salama.