RUWASA kuja na mfumo wa kudhibiti upotevu wa mapato
8 November 2023, 3:07 pm
Baraza la madiwani Nsimbo Mkoa wa Katavi waishauri Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini [RUWASA] kuthibiti Mapato.
Na Betord Chove-Nsimbo
Baraza la madiwani katika halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi wameishauri Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini [RUWASA] kudhibiti mapato yanayokusanywa na jumuiya za watumiaji maji vijijini ili kuendeleza miradi mingine.
Hoja hiyo imebuliwa na madiwani katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kinajadili taarifa za taasisi,na Kata kwenye Halmashauri hiyo ambapo madiwani walibainisha upotevu wa mapato pia mafundi wengi wanaotumika na Ruwasa kutokuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Christian Mpena Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mpanda amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na amesema serikali kwa kutambua hilo wameleta watalaamu kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo ya upotevu wa mapato hayo yanayokusanywa.
Katika Hatua nyingine Mpena amesema kuwa watakwenda kutekeleza mradi wa kubadilisha Pampu za mkono kwenye kwenye visima kijiji cha Masewela,Filimule’ Kabulonge,