Mpanda FM
Uvamizi Misitu: Kilio kwa Sokwe Mtu
30 March 2022, 4:59 pm
Uvamizi wa maeneo ya hifadhi za misitu mkoani Katavi imetajwa kuwa chanzo cha mnyama sokwe mtu kuendelea kupungua.
Josephine Lupia na afisa misitu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa amesema kuwa tabia ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu katika meneo ya hifadhi inapelekea wanyama hao kuhama makazi yao.
Aidha katika hatua nyingine amewataka wananchi kulinda hifadhi na mistu iliyopo katika meneo yanayowazunguka ili kuendelea kuwalinda wanyama pori kutotoweka na kunufaisha maendeleo ya mkoa katika sekta ya utalii.
Mkoa wa katavi unaongoza kwa wingi wa sokwe mtu jumla ya sokwe 1200 ambapo kitaifa ikiwa na jumla ya sokwe mtu 2400.