Kampeni ya TRA ya Tuwajibike Yawagusa Wananchi
12 May 2023, 8:12 am
KATAVI
Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza namna ambavyo wanapaswa kuwajibika katika ulipaji wa Kodi ili kuendelea kushiriki katika kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Wameyaeleza hayo kutokana na kampeni ya Tuwajibike ambayo inafanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Katavi ambapo wamemeeleza namna wanavowajibika kulipa Kodi kupitia mifumo iliyowekwa.
Kwa upande wake meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Katavi Jacob Mtemang’ombe amesema Lengo la kampeni ya Tuwajibike ni kujenga uelewa kwa jamii kutambua umuhimu wa kulipa Kodi.
Mtemangombe amesema kwasasa wanalenga kila Mtanzania ambaye amefikisha umri wa miaka 18 awe na namba ya mlipa kodi (Tin number).