Mpanda FM

Madereva Bajaji Walalamikia Usumbufu Stendi ya Tanganyika

2 May 2023, 9:35 am

KATAVI

Baadhi ya madereva Bajaji wanaofanya safari kutoka Mpanda mjini kuelekea wilaya ya Tanganyika wamelalamikia usumbufu wa kulazimishwa kuingia stendi ili kutoa ushuru.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM madereva wamesema awali walikuwa wakifanya safari bila kulazimika kuingia stendi hiyo huku wakiamini kuwa stendi hiyo inapaswa kutumika na magari na sio chombo kingine cha moto.

Akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesema stendi hiyo inapaswa kutumika na watu wote wanaotumia vyombo vya moto kutokana na abiria kuhitaji huduma zinazopatikana katika stendi hiyo.

Stendi hiyo ipo katika eneo la Majalila wilayani Tanganyika mkoani Katavi.