Joy FM
Joy FM
2 June 2025, 15:32

Wazazi na walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia lishe kwa watoto wao ili waweze kuwa afya bora.
Na Michael Mpunije
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP kupitia mradi wa Kigoma Joint Programme limekabidhi mashine 5 za kuongeza virutubishi kwenye unga wa mahindi katika halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma ili kuongeza hali ya lishe kwa watoto huku Kauli mbiu ikisema kuwa “Wajibika mwanao awe na lishe bora Kwa faida ya wote”
Mashine hizo zimelenga kuwanufaisha wananchi wa halmashauri mji Kasulu katika kukabiliana na utapiamlo kwa watoto hasa waliopo shuleni.

Mkuu wa ofisi ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP wilaya ya Kasulu Saidi Johari ameisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kigoma joint programu( KJP ìì) pamoja na ununuzi wa mashine hizo katika hafla ambyo imefanyika katika shule ya msingi kabanga mazoezi.
Afisa lishe mkoa wa Kigoma James Ngalaba amewatoa hofu wananchi kuacha imani potofu kuhusu mashine za kuongeza virutubish kwenye unga wa mahindi kwakuwa zinalenga kuongeza hali ya lishe kwa watoto.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu Mwl Vumilia Simbeye amelishukuru shirika hilo La mpango wa chakula kwa kutoa mashine hizo na kuahidi kuzisimamia ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kuwanufaisha wananchi wengi zaidi katika kukabiliana na udumavu kwa watoto.

Akiwa mgeni Rasmi katika hafla ya makabidhiano hayo, Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amewataka wazazi na waalimu wa shule za msingi kutambua umuhimu wa mashine hizo ambazo tayari zimefungwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kasulu ili zilete tija kwa watoto pamoja na kuwataka maafisa lishe kubuni mbinu ya namna gani wananchi wengi wanaweza kunufaika na mashine hizo.