Joy FM
Joy FM
14 April 2025, 08:35

Maafisa usafirishaji maarufu Madereva bodaboda wilayani Kigoma wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na vitendo vya ukatili.
Na Kadislaus Ezekiel
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashidi Chuachua amewataka madereva bodaboda kusaidia kudhibiti matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto ikiwa ni pamoja kutoa taarifa za wanaohusika na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dr. Chuachua amesema hayo wakati akiongea na madereva bodaboda katika Kijiji cha Bubango Kata ya Bitale na kuwataka kutojihusisha na usafirishaji haramu na kuwa walinzi wa watoto dhidi ya ukatili.
Aidha Dr. Chuachua amesema Serikali inatambua mchango wa Madereva Bodaboda, na kwamba itawaunga mkono katika kufanikisha wanapata mikopo ya asilimia kumi, ili kuhakikisha wanaongeza juhudi katika kazi na kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao madereva bodaboda wameomba kupatiwa vitambulisho vya nida ili waweze kusoma na kupata leseni za udereva, kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa kuzingatia kanuni na sharia za usalama barabarani.