

6 March 2025, 16:48
Serikali imeendelea kufanya ukarabati waa miundombinu ya majengo katika hospitali mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Na Hagai Ruyagila
Mradi wa ukarabati mkubwa wa hospitali ya halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wa majengo 15 unaendelea vizuri ambapo mpaka sasa tayari majengo 11 yamekarabatiwa baada ya kupewa fedha na serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 900.
Akisoma taarifa ya ukarabati huo, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya Mji Kasulu Dkt Japhari Makombe amesema serikali imesaidia kwa kiasi kikubwa fedha za ukarabati wa majengo ya hospitali hiyo kwani miundombinu yake ya awali ilikuwa hairidhishi huku akibainisha majengo ambayo tayari yameshakarabatiwa.
Dkt Japhari amesema mpaka sasa ukarabati unaendelea na tayari wameshatumia kiasi cha shilingi milioni mia saba hamsini na saba na hamsini na mbili mia tatu tisini na tisa nukta tisa tisa huku salio lililobaki ni shilingi milioni mia moja arobaini na mbili laki tisa arobaini na saba na mia sita.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye amesema halmashauri hiyo itaendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha mazingira ya hospitali hiyo yanaboreshwa ili wananchi wanapata huduma bora.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndg Christopher Palanjo ameihimiza serikali kufanikisha ukarabati huo unakamilika kwa wakati ili kuendelea kuwasaidia wananchi kupata huduma za afya karibu.
Naye Bi. Wifrida Zabron ni mwananchi wa halmashauri ya Mji Kasulu ambaye ameguzumzia namna ambavyo wahudumu wa hospitali hiyo wanavyotoa huduma baada ya mgonjwa kufika hospitalini hapo.
Ukarabati huo wa hospitali ya halmashauri ya Mji Kasulu umeanza mnamo Novemba 2023 na unatarajiwa kukamilika Mwezi April 2025.