

10 February 2025, 11:45
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya wameendelea kuweka mikakati ya kupata suluhisho la tatizo la vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa kuhakikisha huduma za dharula zinapatikana kwenye jamii.
Na Emmanuel Kamangu
Katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto, mfumo jumuishi wa wa usafiri wa dharula wa M-mama unaosaidia mama mjamzito, mama aliejifungua ndani ya siku 42 , pamoja na watoto wa changa walioko chini ya siku 28 umekuja na suruhisho la kuondokana na vifo visivyo vya lazima kwa makundi hayo.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mratibu wa huduma ya usafiri wa dharua kwa mama na mtoto M-mama Halmashauri ya mji kasulu Augustine Karol amesema jumla ya gari nne za kubeba wagonjwa zimetolewa kwa kanda nne za mji kasulu kwa ajili ya kuhudumia wajawazito,mama aliejifungua pamoja na watoto wachanga wenye vidokezo vya hatari.
Aidha Karoli amesema katika kuhakikisha mama mjamzito na watoto wanapata huduma bora za kiafya wamekuja na utararibu wa kuwa na dreva jamii kwa maeneo yote ya mji wa kasulu ili kusaidia kusafisha wagonjwa wanaokumbana na vidokezo hatari vinavyoweza kugarimu maisha yao.
Videkozo hatari kwa mama mjamzito na mbavyo vinapaswa kushugulikiwa kwa wakati ni pamoja na kupata uchungu mapema, kuvimba uso au miguu, maaumivu makali ya kichwa, maumivu makali ya tumbo huku mama mjazito dalili hatari ikiwa ni pamoja na kutokwa damu nyingi ukeni, homa, kuoma giza na watoto wachanga ikiwa ni kushindwa kunyonya, dege dege, kuvimba utosi pamoja na kupatwa joto kali.