

30 January 2025, 15:17
Serikalikatika halmashauri ya wilaya Kasulu imesema itaendelea kusimamia miradi ya maendeleo ili iweze kusaidia wananchi
Na Hagai Ruyagila
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma limepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 35 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Bajeti hiyo imepitishwa katika kikao cha robo ya pili ya mwaka 2024/2025 katika baraza la madiwani
Katika Baraza hilo mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya Kasulu ambaye pia ni diwani wa Kata ya kitanga Mh. Eliya Kagoma amewasisitiza madiwani kuwaeleza wananchi shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali katika maeneo yao.
Aidha Bajeti hiyo imeonekana kugusa maeneo yote muhimu ambayo yanailenga jamii na jambo la msingi ni namna itakavyotekelezwa ili kumsaidia mwananchi wa kawaida. lakini nini maoni ya viongozi wa vyama vya siasa kuhusu Bajeti hiyo??
Diwani wa kata ya Kigembe Simon Mpaka amesema kinachosubiriwa ni kuona ikiwa bajeti hiyo itapitishwa bungeni ili kusaidia shughuli za maendeleo kwenye kila kata.