Joy FM

Viongozi wa vijiji watakiwa kusoma mapato na matumizi

13 January 2025, 13:01

Viongozi wa serikali za vijiji wilayani Kasulu wakiwa katika semina elekezi, Picha na Hagai Ruyagila

Uomaji wa mapato na matumizi kwa wananchi ni miongoni mwa viyu ambavyo vinatajwa kuwa sehemu ya kushawishi wananchi kushiriki kikamilifu kwenye suala la maendeleo kwenye maeneo yao.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Viongozi Serikali za vijiji halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kufanya mikutano na wananchi ili kusoma taarifa za mapato na matumizi pamoja na kujadili hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji vyao.

Wito huo umetolewa na Afisa serikali za mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw Hussein Moshi wakati akizungumza na radio Joy na kueleza kuwa  wenyeviti wa vijiji na watendaji wao wanapaswa kufanya mikutano na wananchi ili kujadili maendeleo ya vijiji vyao.

Afisa serikali za mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw Hussein Moshi, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema moja ya sababu zinazochangia baadhi ya wananchi kushindwa kuhudhuria mikutano ya vijijii ni pamoja na viongozi wao kushindwa kusoma mapato na matumizi kwa muda mrefu pamoja na kushindwa Kushirikisha wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Sauti ya Afisa serikali za mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw Hussein Moshi

Akifunga Semina elekezi kwa Wenyeviti wa vijiji na vitongoji, Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu amewataka viongozi wa vijiji kufuata sheria na kanuni za uongozi huku akisistiza suala la kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi kwa ajili ya kuimarisha usalama.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila
Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu

Baadhi ya wenyeviti wa Vitongoji waliohudhuria semina hiyo wamesema viongozi wanapaswa kujitathmini wanapoona mwitikio mdogo wa wananchi kwenye mikutano yao na kuangalia namna bora ya kuwashirikisha katika Shughuli za maendeleo kabla miradi haijaanza kutekelezwa na kuwataka wananchi kushiriki mikutano hiyo ili kujadili maendeleo na changamoto za kijiji.

Sauti ya Baadhi ya wenyeviti wa Vitongoji waliohudhuria semina hiyo