DED Buhigwe atakiwa kusimamia ujenzi sekondari Kahimba.
10 January 2025, 12:39
wakati shule zikitarajiwa kufunguliwa wiki ijayo jumatatu ya januari 13 ambapo maelengo ya serikali ni kuhakikisha miundombinu ya madarasa inakuwa tayari na wanafunzi kuanza kuyatumia.
Na Josephine Kiravu.
Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe kuhakikisha ujenzi wa miundombinu katika shule ya Sekondari ya wasichana Kahimba unakamilika kwa wakati ili kuruhusu kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Katibu tawala ametoa maelekezo hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo sambamba na kujionea maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka huu wa 2025 katika shule hiyo.
Sauti ya Katibu tawala mkoa wa kigoma.
Hata hivyo katibu tawala amemsisitiza Mkurugenzi huyo kuhakikisha anawaelekeza wakandarasi kuongeza idadi ya mafundi ili kukamilisha kazi zinazotakiwa kufanyika kwa wakati.
Sauti ya katibu tawala
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo George Mbilinyi amemuhakikishia Katibu Tawala kuwa hatosita kuchukua hatua dhidi ya mkandarasi yeyote atakayeshindwa kuzingatia matakwa ya kimkataba na kukwamisha kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa.
Hayo yanajili wakati shule zikitarajiwa kufunguliwa wiki ijayo jumatatu ya januari 13 ambapo maelengo ya serikali ni kuhakikisha miundombinu ya madarasa inakuwa tayari na wanafunzi kuanza kuyatumia.