Wazazi na walezi watajwa chanzo cha kuharibu ushahidi mahakamani kesi za ukatili
3 December 2024, 14:39
Wazazi na walezi wametakiwa kutokuwa sehemu ya kukwamisha na kuharibu ushahidi dhidi ya watau wanaotekeleza vitendo vya ukatili kwenye jamii.
Na Josephine Kiravu
Tukiwa katika muendelezo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Hakimu mfawidhi mahakama ya mkoa wa Kigoma Aristida Tarimo amewataka wazazi kutokuwa chanzo cha kuharibu ushahidi mahakamani kwani kufanya hivyo ni kukwamisha kesi na kuwapa nguvu watuhumiwa wa vitendo hivyo vya ukatili.
Ukatili wa kijinsia unatajwa kuwa janga kubwa, na miongoni mwa changamoto zinazotajwa kuchangia ni pamoja na ucheleweshaji wa kesi,mila na desturi potofu pamoja na uwepo wa sheria kandamizi.
Na hapa hakimu Aristida anaanza kwa kueleza mambo ambayo mara kadhaa yanakwamisha kesi hizi zinapofika mahakamani.
Lakini je mambo gani muhimu ya kuzingatia unapofanyiwa ukatili wa kingono?
Hata hivyo baadhi ya wazazi wamekuwa na mtazano tofauti kuhusu baadhi ya wazazi/walezi ambao wamekuwa wakiharibu ushahidi mahakamani.
Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hufanyika kuanzia Novemba 25 hadi disemba 10 na kwa mwaka huu kampeni hiyo inaongozwa na kauli mbiu isemayo Kuelekea miaka 30 ya Beijing: Chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia.