Joy FM

FDC Kasulu yaomba serikali kukamilisha jengo la kituo cha kulea watoto

7 November 2024, 12:41

Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtelewe akimkabidhi mkuu wa chuo Cha maendeleo ya wananchi Kasulu FDC mifuko ya saruji, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha wanasaidia kukamilisha ujenzi wa jengo la kulea watoto lililopo katika chuo cha maendeleo ya wananchi Kasulu FDC.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Mkuu wa chuo cha maendeeo ya wananchi Kasulu FDC mkoani Kigoma Bi. Fridegard Mukyanuzi ameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa jengo la kituo cha kulea watoto wadogo mchana (Day Care) katika chuo hicho ili kuweka mazingira bora ya kuwaandaa watoto na kuwalea katika maadili mema.

Bi. Mukyanuzi amesema wameenga kufika mwezi januari mwaka 2025 jengo hilo liwe limekamilika ili kuanzisha kituo cha kulelea watoto kutoa malezi na makuzi ya mtoto.

Amesema wana ukosefu wa mifuko 50 ya saruji ambayo imepelekea jengo hilo kusimama na kwamba ikiwa serikali itatatua changamoto hiyo itasaidia ujenzi huo kukamilika kwa wakati.

Mifuko ya saruji iliyotolewa na Katibu tawala wilaya Kasulu kwa mkuu wa chuo cha FDC Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mkuu wa chuo cha maendeeo ya wananchi Kasulu FDC mkoani Kigoma Bi. Fridegard Mukyanuzi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Mwl. Vumilia Simbeye ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu ameiunga mkono serikali kwa kutoa mifuko 20 ya Saruji kuhakikisha changamoto hiyo inapata suluhu.

Mwenyekiti wa bodi ya chuo Cha maendeleo ya wananchi FCD Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Mwl. Vumilia Simbeye ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu

Naye Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele ametoa mifuko 50 ya saruji ili kufanikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa wakati uliokusudiwa.

Sauti ya Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele
Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele, Picha na Hagai Ruyagila