Wananchi watakiwa kutumia maji safi kuepuka kipindupindu Kigoma
6 November 2024, 09:35
Wananchi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, wametakiwa kutumia maji safi na salama kwa matumizi ya kunywa kutoka kwenye vyanzo sahihi vya maji ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu.
Hayo yamesemwa na afisa afya Mkoa wa Kigoma Bw. Nesphori Fikiri Sungu wakati akizungumza na Radio Joy Fm ambapo ameeleza kuwa kumekuwepo na mlipuko wa kipindupindu sababu zikitajwa kuwa ni wananchi kutumia vyanzo vya maji visivyokuwa safi na salama.
Bw. Sungu amesema viongozi wote wa kaya mkoani kigoma hawana budi kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora kama sehemu ya kuendelea kulinda afya za watu wengine.
Hata hivyo amesema kuwa halmashauri ya wilaya kigoma imekuwa ikitoa visa vingi vya ungonjwa kipindupindu huku ikiwa kata ya kitongoni na kata ya majengo zimetoa wagonjwa wawili.