Joy FM

Bilioni 16 kujenga soko la kisasa Mwanga, mwalo Katongo Kigoma

4 November 2024, 08:33

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa, TAMISEMI Zainabu Katimba, Picha na Lucas Hoha

Serikali imesema itaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali na huduma za jamii ili kusaidia kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Na Lucas Hoha – Kigoma

Zaidi ya shilingi bilioni 16 zimetengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa Soko la kisasa la Mwanga na Mwalo wa katonga Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkoani Kigoma ujenzi ambao unaoanza novemba 15 mwaka huu na unatarajia kukamilika Novemba 14 mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa, TAMISEMI Zainabu Katimba, wakati wa utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa Soko hilo na Mwalo wa katonga ambapo
amesema mradi huo umefadhiliwa na Banki ya Dunia kupitia mradi wa TACTIC na baada ya ujenzi kukamilika wa soko la mwanga Manispaa inatarajia kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 1 tofauti na awali Manispaa ulikuwa inakusanya Milioni 450 kwa mwaka.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa, TAMISEMI Zainabu Katimba akiwa ameshika mikataba iliyosainiwa ya ujenzi wa soko la mwanga na mwalo wa katonga, Picha na Lucas Hoha

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amesema serikali inaendelea kuufungua mkoa wa Kigoma kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege na barabarani, huku mwakilishi wa TARURA kutoka makao makuu akiwaomba viongozi wa mkoa kusimamia miradi hiyo kikamilifu ili ubora wa miradi iendane na thamani ya fedha iliyotolewa yaani Value for money.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo la kigoma mjini Kilumbe Ng’enda ameishukuru serikali kuanza utekelezaji wa miradi hiyo, huku Meya wa Manispaa hiyo Baraka Naibuha Lupoli akitoa ahadi ya kuongeza fedha zinazotokana na mapato ya ndani ya Manispaa ili mradi huo wa soko ukamilike kwa wakati.

Wanchi wa manispaa ya Kigoma Ujiji waliojitokeza kushuhudia zoezi la utiaji saini mikataba ya ujenzi wa soko la mwanga na mwalo wa kibirizi, Picha na Lucas Hoha

Ikumbukwe kuwa imepita zaidi ya miaka minne tangu soko la Mwanga kuvunjwa na wafanya biashara walihamishiwa soko la Masanga ili kupisha ujenzi wa Soko hilo la kisasa