Mpanda FM

Kamati ya PETS Yabaini Madudu Shule za Msingi Nsimbo

6 April 2023, 9:18 am

NSIMBO

Kamati ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika shule za msingi (PETS) halmashauri ya Nsimbo imebaini uwepo wa uchakavu wa miundombinu,ukosefu wa vyoo mashuleni na uhaba wa walimu.

Akisoma taarifa ya Awali wakati akiwasilisha taarifa ya Mrejesho wa [PETS] kwa kata zinazonufaika na mradi huo unaotekelezwa na shirika la Green Leaf kwa Ufadhili wa Foundation for civil society Joyce Benedictor mwenyekiti wa PETS amesema kuwa bado serikali inapaswa kuboresha miundombinu ya elimu msingi ili kuweka mzingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Nsimbo Erimkwasi Jonh amesema kuwa Mradi wa PETS Tangu uanze kutekelezwa umekuwa na manufaa kwa wananchi na halmshauri kwa kuwaongezea uelewa watendaji wa serikali na wananchi juu ya kutimiza wajibu wao na uwajibikaji kwenye shule zao.

Mradi wa ushiriki na ushirikishwaji wa matumizi ya fedha za umma katika shule za msingi halmshauri ya Nsimbo unatekelezwa katika shule nane zilipo kata nne Kanoge,Katumba,Kapalala na Nsimbo ambapo mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 39.