Wananchi Waomba Elimu Zaidi Juu ya Kifua Kikuu
27 March 2023, 5:28 pm
Mpanda
Zikiwa zimepita siku chache tangu yafanyike maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani Baadhi ya wakazi manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema kuwa hawana uelewa juu ya ugonjwa huo na kuitaka serikali kuongeza jitihada za kutoa elimu.
Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti wananchi wamesema kuwa hawana ulewa namna unavyo ambukiza dalili, na matibabu yake jambo ambalo wamesema linachangia kutokuona umuhimu wakufika katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupatiwa huduma
Kwaupande wake Mratibu wa huduma za kifua kikuu na Ukoma Manispaa ya Mpanda DR Bruno crnonwel akizungumza na kituo hiki juu ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo amesema kua asilimia kubwa ya wagonjwa wamekuwa wakifika katika vituo vya kutolea huduma wakiwa wameshapata madhara makubwa
Ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao huambukizwa kwa njia ya hewa na moja ya dalili zake ni pamoja na kutokwa jasho wakati wa usiku ,mwili kupungua uzito sambamba na kuugua kikohozi zaidi ya wiki tatu