Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Wanawake Waaswa Kupinga Vitendo vya Ukatili
9 March 2023, 1:08 pm
KATAVI
Katika kuelekea siku ya mwanamke Duniani march 8 mwaka huu ,Wanawake Mkoani Katavi wametakiwa kupinga vitendo vya uvunjifu wa maadili sambamba na vitendo ukatili kwa wanawake na watoto ili kuendelea kutengeneza jamii yenye maadili na usawa
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati wa kongamano la wanawake lililofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda na kusema kuwa mwanamke anayo nafasi kubwa ya kuhakikisha vitendo vya ndoa za jinsia moja na ubakaji vinaisha katika jamii kwa kuendeleza malezi yanayotokana na dini
Kwa upande wao washiriki wa kongamano hilo wamesema kuwa vitendo hivyo vianapaswa kuendelea kupingwa kwa nguvu moja ili kuendelea kuitengeneza jamii yenye madili
Kilele cha siku ya wanawake duniani kinatarajia kufanyika marchi 8 mwaka huu katika wilaya ya Tanganyika ,viwanja vya shule ya msingi Majalila ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa