Mpanda FM

Uhujumu Miundombinu Chanzo cha Huduma Mbovu za Maji na Umeme Katavi

9 March 2023, 1:04 pm

KATAVI

Uhujumu wa miundombinu Imetajwa  kuwa  sababu inayopelekea Kupunguza utoaji huduma bora  kwa Jamii Mkoani Katavi kwa shirika la Umeme Tanzania [Tanesco] na Mamlaka ya maji  safi na  usafi wa Mazingira Mpanda [MUWASA].

Wakizungumza  wakati wakitoa makadirio ya bajeti za mamlaka zao kwa mwaka wa kiserikali 2023/2024 wakurugenzi  wameainisha changamoto hizo ambazo wananchi wenye nia ovu wamekuwa wakiiba miundombinu hiyo na kuiuza kama chuma chakavu hali inayopelekea kupunguza ufanisi katika kutoa huduma.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Ali hamad Makame amesema jeshi linawashikilia watuhumiwa wa matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani na kuwataka wananchi pamoja na mamlaka kutoa ushirikiano katika kuendelea kuwabaini waharibifu wa miundombinu ya serikali.

Katika Hatua nyigine mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwamavua Hoza Mrindoko Amewaonya wafanyabiashara wa chuma chakavu mkoani Hapa kusitisha kununua vyuma ambavyo ni miundombinu nya serikali na kusema atasitisha biashara hiyo ikiwa wataendelea kuhujumu miundombinu ya serikali.