Kupanda kwa Bei ya Mafuta Kilio kwa Abiria Katavi
4 March 2023, 5:54 pm
KATAVI
Abiria wa vyombo vya moto mkoani Katavi wameiomba serikali ipunguze bei ya mafuta kwani hali hiyo ina athiri shughuli zao za kila siku.
Wakizungumza na mpanda Radio fm abiria hao wamesema kuwa kwa sehemu walizokua wakienda kwa Shilingi mia tano wanatumia shilling elfu moja hali ambayo inaleta ugumu kwa abiria hao.
Kwa upande wa madereva wa Bajaji wamesema wanakua na wakati mgumu kuwaelimisha baadhi ya abiria juu ya suala zima la kupanda kwa bei ya mafuta kwani kuna wanaokuwa hawaelewi pindi bei ya mafuta inapopanda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Nidhamu wa madereva wa Bajaji kituo cha TEMESA amewaomba abiria kuendelea kuzoea bei hizo kwani ndiyo hali halisi ya bei ya mafuta kwani bidhaa hiyo imekuwa ikitoka nje ya nchi.
Kila Jumatano ya kwanza ya Mwezi ,serikali utangaza bei ya Mafuta ambapo kwa Manispaa ya Mpanda Bei ya mafuta ya petrol kwa lita ni sh 3125,huku dizeli ikiwa sh 3288 kwa lita, na mafuta ya taa ni sh 3256 kwa lita.