Tayobeco Yaendelea Kuhamasisha Chanjo ya Uviko 19.
4 March 2023, 5:09 pm
MPANDA.
Shirika lisilo la kiserikali la Tayobeco Linalojihusisha na kuboresha afya ya vijana katika Nyanja mbalimbali Limezindua Mradi wa boresha habari katika manispaa ya mpanda Mkoani katavi lengo ni kuhamasisha vijana na wanawake kujitokeza katika kupata chanjo ya uviko 19.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mradi huo Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Shida Kabulunge amesema wamejikita katika kutoa elimu na hamasa kwa jamii ili wananchi wajitokeze na kuendelea kupata chanjo dhidi ya uviko 19 .
Adidani Musa ni msimamizi wa program hizo amesema mradi huo umewalenga vijana na wanawake katika kuwahamasisha na kutoa elimu zaidi juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya uviko 19 lakini pia hawataishia kwa makundi hayo pekee.
Kwa upande wake mratibu wa huduma za chanjo manispaa ya Mpanda Ibrahim Mikidadi amewataka wadau mbalimbali kujitokeza katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo ya uviko na chanjo za watoto