Mpanda FM

7 February 2023, 10:21 pm

MPANDA

Baadhi ya kinamama wanaopata huduma ya matibabu katika kituo cha afya ilembo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa pongezi kwa watoa huduma katika kituo hicho kwa kubainisha kuwa huduma zinazotolewa zinakidhi mahitaji .

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm akinamama hao wamepongeza uwepo wa lugha rafiki baina ya wagonjwa na watoa huduma jambo ambalo wamesema linawafanya kuvutiwa kupata huduma za kimatibabu katika kituo hicho

Kwa upande wake Mganga mkuu Manispaa ya Mpanda Paul Swakala amesema kituo hicho kinapata wateja wengi wanaotoka maeneo mbalimbali na kusema kuwa hali hiyo inawalazimu wahudumu kufanya kazi masaa 24 huku akibainisha kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti.

Kituo hicho cha afya kimetoa huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito zaidi ya mia tisa kwa mwaka 2022 huku zaidi ya kinamama elfu nne wakipata huduma katika kituo hicho .