Mpanda FM

Kilio Watendaji Uuzaji Pombe Muda wa Kazi

17 January 2023, 5:49 pm

MPANDA
Baadhi ya wananchi Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema kuwa kuendelea kuwepo kwa wafanyabiashara wanaofungua kumbi za starehe na pombe kinyume na muda uliopangwa unachangiwa na watendaji wasio wajibika katika usimamizi wa sheria

Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wamesema watu wanaojikita katika unywaji wa pombe muda wa kazi wanachangia kutengeneza migogoro katika familia pamoja na hali duni ya kimaisha.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu amesema wananchi wanaofanya biashara ya kuuza pombe muda wa kazi ni kinyume cha sheria na taratibu hivyo wametakiwa kuacha kufanya hivyo ili kuruhusu watu kuendelea na majukumu ya ujenzi wataifa .

Mkuu wa wilaya ya mpanda amewataka viongozi wa serikali za mitaa na watendaji kusimamia vyema sheria hizo ili kuepusha ukiukwaji unaofanywa na baadhi ya wananchi.