Mpanda FM

Bei za mafuta zapokelewa Kwa mikono miwili Katavi

8 December 2022, 5:33 pm

MPANDA
Madereva wa vyombo vya moto Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani katavi wametoa maoni yao juu ya mwenendo wa kushuka na kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol na dizel.

Wakizungumza na Mpanda Radio fm kwa nyakati tofauti madereva hao wameishukuru serikali kwa namna ambavyo imeendelea kushusha bei za mafuta hasa mafuta ya pertoli ambayo wamesema yanatumika kwa asilimia kubwa .

Aidha madereva hao wameiomba serikali kuendelea kushusha bei ya nishati nyingine ikiwemo mafuta ya dizeli ili kuendelea kuleta unafuu wa maisha kwa watumiaji wa nishati hiyo .

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zitaanza kutumika tangu December 7 mwezi huu ambapo kwa manispaa ya Mpanda mafuta ya petroli yatauzwa kwa bei elekezi ya sh 2985 huku dizeli ikiuzwa sh 3405.