Wakuu wa Wilaya wapewa maagizo ya kuwaondoa wananchi waliovamia hifadhi pamoja na vyanzo vya maji kuondolewa
25 November 2022, 4:37 am
MPANDA
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua hoza Mrindoko amewaagiza wakuu wa wilaya , kuhakikisha wananchi wote waliovamia maeneo ya hifadhi pamoja na vyanzo vya maji wanaondoka katika maeneo hayo.
Agizo hilo amelitoa katika kikao cha 19 cha kamati ya ushauri mkoa, na kusema kuwa kuendelea kuwepo kwa wanachi wanaokaa katika maeneo ya hifadhi pamoja na maeneo ya vyanzo vya maji ni kinyume na sheria.
Sambamba na hilo Mrindoko amezungumzia suala la usafi wa mazingira ambapo amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika zoezi la usafi ili kujiepusha na magonjwa katika kipindi hiki cha masika.
Kikao hicho cha kamati ya ushauri wa mkoa hufanyika mara moja kila mwaka lengo likiwa ni kujadili maswala mbalimbali ya maendeleo yanayofanyika katika mkoa.