Katavi :Wanahabari na wadau wa utamaduni Wametakiwa kuibua Urithi wa Utamaduni
12 November 2024, 12:17 pm
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Katavi ,wadau wa utamaduni pamoja na wakufunzi kutoka TAMCODE.picha na Betord Chove
vijana wanaachana na dhana ya kutegemea ajira serikalini na kujishughulisha na vitu vyao vya asili kujipatia kipato
Na Betord Chove -Katavi
Wanahabari na wadau wa utamaduni mkoani Katavi Wametakiwa kuibua Urithi wa Utamaduni usioshikika ili kuvutia wawekezaji na kukuza fursa za kiuchumi
Akifunga mafunzo ya Siku mbili , Ofisa utamaduni Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza, akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda amewataka wadau wa utamaduni na wanahabari kuyafanyia kazi kwenye jamii.
Sauti ya Ofisa utamaduni Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza, akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari na wadau wa utamaduni wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa ili kuhakikisha jamii hususani wanawake na vijana wanaachana na dhana ya kutegemea ajira serikalini na kujishughulisha na vitu vyao vya asili kujipatia kipato
Sauti ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari na wadau wa utamaduni
Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (Tamcode) kupitia Mfuko wa UNESCO- Alwaleed Philanthropies.