Mpanda FM

Wananchi wilaya ya Tanganyika Wajitokeza Kupata Chanjo ya Uviko-19

3 November 2022, 5:29 am

KATAVI

Baadhi  ya wananchi  wa Luhafe wilayani Tanganyika wamejitokeza kupata chanjo ya uviko 19 kijijini hapo, inayoratibiwa na taasisi ya Benjamini Mkapa.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi waliopata chanjo ya Uviko 19, wameishukuru serikali pamoja na wadau kwa kuwapelekea chanjo bure kijijini hapo, huku wakisema kuwa chanjo hiyo haina madhara yeyote mwilini kama baadhi yao wanavyodhani.

Zawadi Erinest ni Afisa miradi kutoka taasisi ya Benjamini Mkapa amesema kuwa wamepokea fedha kutoka wizara ya afya kwaajili ya utekelezaji wa kampeni za chanjo ya Uviko -19  kwenye mikoa 10 ikiwemo Katavi.

Naye Mratibu wa chanjo wilayani Tanganyika Philipo Mihayo ameeleza mafanikio waliyoyafikia kwenye zoezi hilo mpaka hivi sasa.

Kampeni ya chanjo ya Uviko 19 ilianza  october 24, na  kabla ya kampeni mkoa ulikuwa na 36% ya watu waliochanjwa na  kufikia october 30 halmashauri ilifikia 64% sawa na watu  Therathini na mbili elfu (32,000).