Wazazi Waaswa Kuwajibika kwa Malezi ya Watoto, Kuepusha Mimba za Utotoni
21 October 2022, 11:15 am
KATAVI
Wazazi mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanawajibika katika malezi ya Watoto wao ili kuepusha kutokea kwa mimba za utotoni.
Wakizungumza na Mpanda radio fm baadhi ya wakazi mkoani hapa wamesema mimba za utotoni mara nyingi zinatokea pindi kukiwa hakuna misingi bora ya malezi ya Watoto.
Tiame Kiame ni Afisa ustawi mkoa wa Katavi amekiri kuwa wazazi na walezi ndio sababu kubwa ya kutokea kwa mimba za utotoni.
Tiame ameongeza kuwa ili kuwalinda Watoto juu ya mimba za utotoni wamekuwa wakiunda kamati za kuhakikisha ulinzi dhidi yao Pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa yeyote atakayehusika kusababisha mimba za utotoni.
Mimba za utotoni zinahusu Watoto wenye umri chini ya miaka 18 ambao wamepata ujauzito, na Mkoa wa Katavi kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018 unaongoza kwa mimba za utotoni ukiwa na asilimia 45.