Wawili wanaswa na bangi 110kg Tanganyika
24 May 2024, 9:19 am
“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na shuguli za dawa za kulevya” Picha na John Benjamin
Na john Benjamin-Katavi
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani Katavi imekamata Kilogramu 110 za bangi na kuteketeza hekari 3 za mashamba ya bangi wilayani Tanganyika.
Akisoma taarifa hiyo afisa sheria kutoka udhibiti dawa za kulevya nyanda za juu kusini Denastus Mnyika amesema kuwa oparesheni hiyo iliyofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 23 mwezi huu katika Kijiji cha Kafisha kata ya Ikola Tarafa ya Karema wilaya ya Tanganyika mkoani hapa na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili Luchagula Minimini Nchoji na Lugiko Salu Sida kwa kuhusika na usafirishaji wa kiasi hicho cha dawa za kulevya.
Sauti ya afisa sheria kutoka udhibiti dawa za kulevya nyanda za juu kusini Denastus Mnyika
Maafisa wa jeshi la polisi wakishirikiana katika kuteketeza mashamba ya bangi yaliyogundulika katika Tarafa ya Karema Kata ya Ikola wilayani Tanganyika. Picha na John Benjamin
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na shuguli za dawa za kulevya huku akiwaomba kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa watu ambao wamekuwa wakijihusisha na kilimo na biashara za wa dawa hizo za kulevya.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu
Baadhi ya wananchi wilayani humo Tanganyika wamepongeza mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini Tanzania kufanikiwa kudhibiti dawa hizo na wameitaka hatua za ziada zichukuliwe kunusuru ili kupunguza athari zinazotokea.
Sauti ya baadhi ya wananchi wilayani Tanganyika wakipongeza mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini Tanzania kufanikiwa kudhibiti‘
Moja ya shamba la bangi lililogundulika wilayani tanganyika katika Tarafa ya Karema Kata ya Ikola. Picha na John Benjamin