Mpanda FM

Wananchi Katavi wahofia aliyesimamia mgogoro wao na jeshi kuwageuka

17 May 2024, 2:06 pm

Huenda ametugeuka kwa kuwa eneo lake limeachwa wazi hivyo tunadhani kuwa zipo sababu za yeye kuegemea upande mmoja na kusababisha maeneo hayo kuchukuliwa na jeshi” Alisema mmoja wa wananchi aliehudhuria kliniki hiyo. Picha na Lilian Vicent

Na Lilian Vicent -Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameendelea  na kliniki ya kusikiliza kero  ambapo kumeibuka hoja ya mgogoro  wa muda mrefu wa  mipaka kati ya  Jeshi La Wananchi Tanzania [JWTZ] na wananchi wa  halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Hayo yamejiri katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda ambapo mmoja  wa Wananchi amesema kuwa kiongozi wao waliomchagua  kusimamia mgogoro huo huenda amewageuka kwakuwa eneo lake limeachwa wazi hivyo wanazani kuwa zipo sababu za yeye kuegemea upande mmoja na kusababisha maeneo hayo kuchukuliwa na Jeshi.

Sauti ya mmoja  wa wananchi amesema kuwa kiongozi wao waliomchagua  kusimamia mgogoro huo huenda amewageuka.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Mwanamvua Hoza  Mrindoko amebainisha  kwa taarifa aliyonayo mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu  tayari umemalizika kwa mujibu wa wataalamu  na Wanachi wameshiriki na endapo kuna upande au mtu  hajaridhishwa  na uamuzi huo aende mahakamani.

Sauti ya mkuu wa mkoa Mwanamvua Hoza  Mrindoko akibainisha kuwa taarifa aliyonayo ni kuwa mgogoro huo umekwisha.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amezitaka ngazi zote kuanzia kwa Katibu Tawala Mkoa, halmashauri zote, wakuu wa taasisi na vyombo vya dola kushughulikia kero zote bila kusubiri siku maalum ya kusikiliza kero.

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza  Mrindoko alipokuwa akizungumza kuwa taarifa alionayo ni kuwa mgogoro huo umemalizika. Picha na Lilian Vicent

Pia baadhi ya wananchi wamelalamikia baadhi ya viongozi katika ofisi kuwa na tabia ya ubinafsi katika ofisi za umma, ambao Mwanachi mwingine amemwambia Mkuu wa Mkoa kuwa baadhi ya Watumishi wa Umma wanakwamisha mambo kwa makusudi kwani badala ya kusikiliza na kutatua kero za wanachi wamekuwa na tabia ya ‘Umungu Mtu’ kitendo alichokitaja kama kuigombanisha Serikali na wananchi.