Mpanda FM
WANAWAKE JISHUGHULISHENI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
8 June 2022, 3:47 pm
Wanawake katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujishughulisha ili waweze kujikwamua na umaskini.
Wakizungumza na mpanda radio fm wanawake ambao wanajishughulisha na upetaji wa pumba na kujipatia chenga za mchele na kisha kuziuza wameeleza namna kazi hiyo inavyowasaidia kujikwamua kiuchumi .
Kwa upande wake mmoja wa wanunuzi wa bidhaa hiyo Anastanzia kwanga ameeleza umuhimu wa bidhaa hiyo na kuwataka wanawake ambao hawajishughulishi kufanya kazi ili wajipatie kipato.
Katika jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi serekali inaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake wanaojiunga kwapamoja na kuanzisha shughuli za kimaendeleo zinazowaingizia kipato.