TUWEZESHENI, TUKAWAWEZESHE
8 June 2022, 3:45 pm
Wanachama wa Chama cha wafugaji wa ngombe wa maziwa cha Kashauriri Livestock Keepers kilichopo Wilayani Mpanda wameomba kuwezeshwa na taasisi za fedha kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kutoa fursa ya ajira kwa jamii.
Wakizungumuza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa yaliyofanyika Mkoani Katavi wanachama hao wamesema wamekuwa wakiomba mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha ili kukuza chama hicho na kujenga kiwanda kwa lengo la kutoa fursa ya ajira lakini taasisi hizo zimekuwa zikishindwa kuwawezesha kwa wakati.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua mrindoko kufuatilia jambo hilo ili wanachama hao wawezeshwe kupata mikopo kwa haraka zaidi.
Chama cha wafugaji wa ngombe wa maziwa cha Kashauriri Livestock Keepers kilianzishwa mwaka 2006 kikiwa na lengo lakufanya ufugaji wenye tija.