TAKUKURU Katavi kufuatilia miradi ya shilingi bilioni 9.57
1 February 2024, 5:27 pm
TAKUKURU wanaendelea kufaatilia utekelezaji wa Miradi 11 yenye thamani ya Shilingi Billioni 9.57 katika sekta ya elimu,Afya na ufundi stadi [VETA].Picha na Gladness Richard
Na Gladness Richard-Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Katavi TAKUKURU wamepokea malalamiko 65,ambayo taarifa za Rushwa ni 35 na siziso za Rushwa 30.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi Faustine Maijo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuwa malalamiko yaliyohusiana na vitendo vya Rushwa yalikuwa yakijumuisha sekta mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa,Kilimo,Polisi TFS na Madini.
Sauti ya Mkuu wa TAKUKURU Katavi Faustine Maijo akitoa taarifa kwa umma kuhusu vitendo vya rushwa vilivyobainika
Hata hivyo Maijo ameongezea kuwa wanaendelea kufaatilia utekelezaji wa Miradi 11 yenye thamani ya Shilingi Billioni 9.57 katika sekta ya elimu,Afya na ufundi stadi [VETA].
Sauti ya Mkuu wa TAKUKURU Katavi Faustine Maijo akitoa taarifa kwa umma kuhusu ufuatiliaji wa miradi.
Aidha amesema TAKUKURU itaendelea kuimarisha juhudi za kuzuia Rushwa kwa kuendelea kufuatilia utelekezaji wa Miradi ya maendeleo, makusanyo na uwasilishaji wa mapato yanayotokana na mashine za P.O.S na kuwachukulia hatua kali za kishaeria wale watakaobainika kufuja mali za umma na kutofuata miongozo ya fedha.