Wiki ya Sheria Wananchi Mjitokeze Kupata Elimu
24 January 2024, 3:24 pm
“Hakimu Mfawidhi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi amewaasa Wananchi kujitokeza kushiriki ili kupata Elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu sheria ” Picha na Festo Kinyogoto.
Na Festo Kinyogoto-Katavi
Kuelekea maazimisho ya wiki ya sheria Hakimu Mfawidhi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi amewaasa Wananchi kujitokeza kushiriki ili kupata Elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu sheria pamoja na msaa wa kisheria.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm Mahakamani hapo ambazo amesema wiki hiyo itakayoanza tarehe 24 na watapita maeneo mbalimbali ya mikusanyiko kwaajili ya kutoa elimu kuhusu msuala ya sheria pamoja na msaada wa kisheria katika Magereza,Shule kadhalika Mabanda yatakakayokuwa Mahakama ya mwanzo Mjini Mpanda na Wilaya zote mkoani Katavi.
Aidha Sumaye amesema Wananchi wanapaswa kuondokana na dhana yakuogopa Mahakama kwani Mahakama ni sehemu ambayo watu wanakwenda kupata msaada wa masuala ambayo yanawatatiza ikiwemo haki za msingi, na amesema dhana hiyo inaendelea kupungua kutokana na Elimu inayoendelea kutolewa katika maadhimisho ya wiki ya sheria.
Sauti ya Hakimu Mfawidhi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi akieleza kuhusu wanancchi kutoogopa Mahakama kwani ni eneo la utoaji haki.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi ambapo yatafanyika maazimisho ya kilele cha wiki ya sheria.
Wiki ya sheria itanza January 24 na kilele chake ni Ferbuay mosi ikiogozwa na kaulimbiu isemayo “Umuhimu wa Dhana ya haki kwa Ustawi wa Taifa nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki Jinai”