Utoro wawakosesha 400 mtihani darasa la nne shule ya msingi Nyerere
20 January 2024, 1:52 pm
Picha na Mtandao
Wanafunzi hao hawakuweza kufanya mtihani wao wa darasa la nne kwa sababu za utoro ziliopelekea kushindwa kufika katika chumba cha kufanyia mtihani.
Na Asha Bakari-Katavi
Zaidi ya wanafunzi mia nne [400] wa Shule ya Msingi Nyerere wameshindwa kufanya mtihani wao wa kujipima uwezo wa darasa la nne sababu kubwa ikitajwa kuwa ni utoro sugu unaofanywa na wanafunzi hao.
Akizungumza na Mpanda Radio FM Mkuu wa idara ya elimu Msingi na awali katika Manispaa ya Mpanda, Mwalimu Godfrey Cosmas Kalulu, amesema kuwa wanafunzi hao hawakuweza kufanya mtihani wao wa darasa la nne kwa sababu za utoro ziliopelekea kushindwa kufika katika chumba cha kufanyia mtihani .
Ameelezea kuwa Watoto 1065 walisajiliwa kufanya mtihani wa kujipima wa Darasa la nne katika shule hiyo ya Msingi na waliofanya mtihani walikuwa 608 huku Wanafunzi 457 kushindwa kufanya Mtihani huo.
Sauti ya Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na awali katika Manispaa ya Mpanda, Mwalimu Godfrey Cosmas Kalulu akieleza sababu za wanafunzi hao kutojitokeza kufanya mtihani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sofia Juma Kumburi ametoa rai kwa ustawi wa jamii na watendaji wa kata Pamoja na mitaa kuendelea kuwasaka na kuwarudisha Watoto shuleni ili kuondoa tatizo la Watoto kutokufanya mitihani.
Sauti ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sofia Juma Kumburi akitoa rai kwa watendaji kuwasaka watoto hao warudi shuleni.
Aidha Kumbuli amesema serikali imetenga zaidi ya Miliomi mia moja na Arobaini 140 kwa Manispaa ya Mpanda kwaajili ya kuongeza vyumba vya Madarasa pamoja na Madawati.