Mpanda FM

VIJIJI SABA KUNUFAIKA NA UPATIKANAJI WA MAJI KATAVI

26 May 2022, 1:27 pm

Vijiji saba vilivyopo ndani ya Wilaya ya Mpanda    mkoani katavi vitanufaika na upatikanaji wa maji kupitia Wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) katika mwaka wa fedha 2022/23.

Akizungumza na Mpanda Radio FM Meneja wa RUWASA Wilayani Mpanda Eng. Christian amesema visima tisa vinachimbwa na RUWASA na kunufaisha vijiji saba Wilayani Mpanda.

Mpena ameongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili Wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini ni pamoja na uvamizi wa vyanzo vya maji na baadhi ya wananchi kutotoa gharama za upatikanaji wa maji.

Kwa mujibu wa mpena amesema Maji ni muhimu kwa viumbe hai hivyo kwa pamoja hatuna budi kulinda na kutunza vyanzo hivyo .