DC Tanganyika akanusha wanafunzi kuchangishwa mifuko ya saruji, madawati
16 January 2024, 10:11 am
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza na wanafunzi .Picha na Deus Daudi
Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii haina ukweli wowote na wanafunzi waendelee kufika shuleni .
Na Deus Daudi-Katavi
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii juu ya Shule ya sekondari Kabungu kupokea Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kuchangisha mifuko ya Saruji na Madawati ambayo ni Kinyume na Matakwa ya Serikali .
Hayo ameyazungumza alipotembelea katika Shule hiyo iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi na kusema kuwa Mwanafunzi atapokelewa katika Shule hiyo bila ya kuwepo na vikwazo vya aina yeyote na hivyo Wazazi waendelee kupeleka Watoto wao Shule kwani kasi ya kuripoti kwa wanafunzi hao hairidhishi
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza shuleni hapo.
Wanafunzi Shule ya Sekondari Kabungu Wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanganyika .Picha na Deus Daudi
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Abdallah Kombo Dawa amesema kuwa Wanafunzi walioripoti mpaka hivi sasa ni 30 huku akieleza taarifa inayosambaa kwenye Mitandao ya kijamii haina ukweli wowote na Wanafunzi waendelee kufika Shuleni hapo.
Sauti ya Mkuu wa Shule Ya Sekondari Kabungu AKieleza idadi ya wanafunzi walioripoti shuleni hapo