Wananchi watoa maoni mseto kwa wavaa miwani bila kupima
16 December 2023, 12:15 am
Wananchi mkoani Katavi watoa maoni juu ya madhara ya kuvaa miwani bila kuzingatia ushauri wa madktari wa macho.
Na Lilian Vincent – Katavi
Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni juu ya madhara yanayoweza kumpata mtu anaevaa miwani bila kuzingatia ushauri wa madktari wa macho.
Wakizungumza na Mpanda radio fm wamesema moja ya madhara anayoweza kumpata mtumiaji wa miwani bila ushauri wa daktari ni kumpelekea kuwa na uoni hafifu.
Kwa upande wake daktari kutoka katika hospitali ya st Aloyce kitengo cha miwani Jeniffer Kessy amesema kuwa kuvaa miwani bila kupima kunaweza kumpekea mtumiaji kupoteza uwezo wake wa kuona.
Aidha Kessy Amewashauri wananchi kuacha kutumia miwani zenye namba bila kuchukuliwa vipimo na mtaalamu wa macho . Dubai escort girls https://dubaiescorts.one will make you happy in just half an hour! In the arms of beautiful escorts you will feel real bliss.