Mbunge Kakoso awakataa madereva walevi
21 November 2023, 10:34 pm
Mbunge Kakoso ameshauri halmashauri hiyo kufanya marekebisho ya magari yaliyoharibika ili yaweze kuendelea kutoa huduma.
Na Anna Milanzi -Katavi
Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini mkoani Katavi amekabidhi gari mpya ya wagonjwa kwa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika huku akisisitiza kuajiri madereva walio na weledi katika kazi.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi gari hilo la wagonjwa mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso amemwomba mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema gari hilo ikiwemo kuajiri madereva wasio walevi.
Kadhalika na hilo Mbunge Kakoso ameshauri halmashauri hiyo kufanya marekebisho ya magari yaliyoharibika ili yaweze kuendelea kutoa huduma.
Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo wakishuhudia Makabidhiano ya Gari hiyo ya Wagonjwa.Picha na Anna Milanzi
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Shaban Juma wakati akikabidhiwa Gari hiyo ameishukuru Serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwapatia Gari hiyo na kuahidi kumpatia Dereva Makini .
Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
Mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika Shaban Juma akizungumza ,huku upande wa kushoto ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Tanganyika Alex Mrema na Upande wa kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini
Mkuu wa Wilaya hiyo Onesmo Buswelu kupitia Vyombo vya Usalama ameahidi kufuatilia Madereva wasiozingatia weledi katika kazi zao.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya Ya Tanganyika
Wananchi wa wilaya ya Tanganyika wakishuhudia Gari Mpya ya Wagonjwa iliyokabidhiwa katika halmashauri hiyo.Picha na Anna Milanzi