UMASKINI, CHANZO MIMBA ZA UTOTONI
23 May 2022, 1:42 pm
KATAVI
Umaskini wa kipato umetajwa Kuwa chanzo moja wapo cha kinachopelekea mimba za utotoni kwa baadhi ya familia mkoani katavi.
Wakizungumza na mpanda redio fm baadhi ya wazazi hao wameeleza namna umaskini wa familia unavyosababisha mabinti wengi kupata mimba kabla ya umri, kuwa ni kutopata mahitaji muhimu kutoka kwa wazazi na walezi wanaoishi nao.
Kwa upande wake mratibu wa polisi jamii na dawati la jinsia na watoto mkoa wa katavi inspekta Kelvin Fuime amesema watoto wa kike wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye mahusiano kwa lengo la kujitafutia mahitaji binafsi ambayo wanayakosa nyumbani.
Mkoa wa katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo inaongoza kwa mimba za utotoni ambapo kitaifa inashika nafasi ya kwanza .